Michezo

Fahamu wanawake 10 tajiri zaidi duniani

Fahamu wanawake hawa tajiri zaidi duniani na namna walivyofika katika hatua hiyo ya utajiri wao.

1) Françoise Bettencourt-Meyers

10 richest women in the world Françoise Bettencourt-Meyers (source- YT)

Thamani yake Dola bilioni 49.3, ni mtu wa 15 tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Fobes.

Yeye ni nani?

Ni mfaransa mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L’Oréal ambaye anamiliki 33% ya kampuni hiyo na familia yake.

Mwanamke huyo wa miaka 65 alirithi mali utajiri huo kutoka kwa mama yake Liliane Bettencourt, aliefariki dunia mwezi Septemba mwaka 2017 akiwa na miaka 94.

Wawili hao walizozana kwa miaka kumi kuhusiana na usimamizi wa kampuni hiyo hadi wakafikishana mahakamani mwaka 2007.

Bi Bettencourt-Meyers aliwasilisha kesi mahakamani akihoji kuwa washirika wa karibu na mama yake walikuwa wakimlaghai licha ya hali yake mbaya ya kiafya.

Lakini waliafikiana miaka kadhaa kabla ya kifo cha mama yake.

2) Alice Walton

10 richest women in the world Alice Walton (source YT CBS News Sunday Morning)

Thamani yake : Dola biloni 44.4, thamani ambayo inamuorodhesha katika nafasi ya 17 ya watu tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 69 ni binti wa kipekee wa mwanzilishi wa duka kubwa zaidi la jumla nchini Marekani,Sam Walton.

Hata hivyo tofauti na ndugu zake wawili wa kiume, alijitenga na biashara ya familia na kujiingiza katika biashara ya sanaa na kuwa mwenyekiti wa makavazi ya sanaa nchini Marekani inayofahamika kama Crystal Bridges Museum iliyo na makao yake mjini Bentonville, Arkansas.

3) MacKenzie BezosJeff and MacKenzie

Thamani yakeNi karibudola bilioni 35.6 -ndio thamani yake katika kampuni ya Amazon pekeea, lakini thamani yake halisi inatarajiwa kuwa juu zaidi.

Yeye ni nani?

Mama huyo wa miaka 48 amezaa watoto wanne na mwasisi wa shirika la Amazon, ambaye alimuoa mwaka 1993 walipokua wakifanya kazi pamoja katika hazina ya hedge.

Mkaazi huyo wa California alikua miongoni mwa wafanyikazi wa kwanza wa kampuni ya Amazon, na alijiunga nalo kama mhasibu.

4) Jacqueline Mars

10 richest women in the world Jacqueline Mars (source Forbes)

Thamani yakeNi dolaola bilioni 23.9 – ni mtu wa 33 tajiri zaidi duniani kabla ya enzi ya MacKenzie Bezos ( sawa na wanawake wengine katika orodha inayofuata hapo chini).

Yeye ni nani?

Mwanamama huyu wa miaka 79 ni mzaliwa wa tatu katika familia ya Mars, kampuni kubwa zaidi ya uokaji dunia ambayo alianzishwa na babu yake Frank mwaka 1911.

Alifanya kazi katika kampuni ya familia yake kwa karibu miaka 20 nakuwa katika bodi ya usimamizi wake hadi mwaka 2016.

5) Yan Huiyan

Thamani yake: Dola bilioni22.1, thanai ambayo inamfanya kuwa mwanamke tajiri zaidi nchini China na mtu wa 42 tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 37 anamiliki hisa katika kampuni kubwa ya ujenzi nchini China inayofahamika kama Coutry Garden Holdings, ambayo inaongoza katika biashara ya sekta ya ujenzi China.

Kwa mujibu wa utafiti Country Garden, ilikua kampuni kubwa zaidi ya ujenzi kote duniani mwaka 2016.

Yan Huiyan, amerithi 57% ya hisa ya kampuni hiyo kutoka kwa baba yake.

6) Susanne Klatten

10 richest women in the world Susanne Klatten (source Want to be Rich)

Thamani yake Ni dola bilioni 21, ambayo inamweka katika nafasi ya 46 ya watu tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani?

Ni mtu wa pili kutoka barani Ulaya katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani. Mwanamke huyu raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 56 ana mchanagnyiko wa magari na makampuni ya dawa.

Alirithi 50% ya kampuni ya kutengeneza dawa ya Altana AG wakati wazazi wake walipofariki, huku ndugu yake wa kiume akimiliki 50% ya kampuni ya uundaji magari ya BMW.

Hata hivyo ameifanya kampuni ya Altana kuwa yake binafsi baada ya kununua hisa zote za kampuni zingine kubwa.

7) Laurene Powell Jobs

10 richest women in the world Laurene Powell Jobs (source Town and Country Mag via Getty)

Thamani yakeNi dola bilioni 18.6, thamani inayomfanya kuwa mtu wa 54 tajiri zaidi duniani.

Yeye ni nani ?

Ni mjane wa mwanzilishi wa kampuni kubwa ya teknolojia ya Marekani Apple, Steve Jobs. Familia yake ilimiliki takriban dola bilioni 20bn katika kampuni za Apple na Disney wakati mume wake alipofariki dunia.

Tangu wakati huo, Bi.Laurene mwenye umri wa miaka 55 aliendelea mbele na kukuza utajiri wake kwa kuwekeza sehemu ya fedha zake katika sekta ya habari, kwa kumili hisa nyingi katika jarida la Atlantic , pamoja na uchapishaji wa wa majarida ya Mother Jones na ProPublica.

8) ABIGAIL JOHNSON

10 richest women in the world Abigail Johnson (source Boston Magazine via Reuters)

Thamani yake: Dola za Marekani bilioni 16.4

Yeye ni nani?

Mrithi wa Fidelity Investments ambayo ilianzishwa na babu yake Edward C. Johnson II – na amekuwa mwanamke wa kwanza kuchukua nafasi ya uongozi, Abigail Johnson amejidhihirisha kuwa mmoja wa wanawake wenye nguvu kubwa katika fedha. Tangu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Fidelity Investments mwaka 2014 na wenyekiti mwaka 2016.

9) IRIS FONTBONA

10 richest women in the world Iris Fontbona (source The Santiago Times)

Thamani yake: Dola za Marekani bilioni 16.4

Yeye ni nani?

Ni ndugu wa familia tajiri zaidi nchini Chile, Iris Fontbona alirithi Group kutoka kwa mume wake Andronico Luksic ambaye alifariki mwaka 2005. Alikuwa amejijengea utajiri katika uchimbaji wa shaba na vinywaji, akiachana na biashara zake Fontbona akiwa na watoto watatu Jean-Paul, Andronico na Guillermo Luksic.

Ingawa kampuni hiyo inaendeshwa sana na Andronico, mama huyo mwenye umri wa 76 ameichukua na kuifikisha katika viwango vya hali ya juu.

10) CHARLENE DE CARVALHO-HEINEKEN

10 richest women in the world Charlene de Carvalho-Heineken (source Fortune)

Thamani yake: Dola za Marekani bilioni 15.7

Yeye ni nani?

Charlene de Carvalho-Heineken hakuwa akiandaliwa kuchukua Heineken, bia ya pili kwa ukubwa ulimwenguni. Biashara ya familia ilianzishwa na babu yake Gerard Adriaan Heineken miaka 150 iliyopita, na mwishowe akapita kwa baba yake, Freddy Heineken kama Mkurugenzi Mtendaji wakati baba yake alipofariki mwaka ndipo akachukua nafasi ya uongozi mwaka 2002.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents