Burudani

Feza Kessy atavuka milima na mabonde na kuingia fainali ya Big Brother Africa?

Kama ni soka, timu ya Tanzania sasa hivi inacheza ikiwa nusu uwanjani. Baada ya kuondolewa kwa Nando jana kwenye shindano hilo kutokana na kuvunja sheria za shindano hilo, Tanzania sasa imebakiza mshiriki mmoja, Feza Kessy.

374442_500432656704965_690117850_n

Feza ndiye mshiriki anayeendela kuyashikilia matumaini ya Watanzania kuwa kama Mungu akipenda, arudi nyumbani na dola laki tatu. Si jambo rahisi lakini kwakuwa mchezo ndio kwanza umekuwa mgumu na kila nchi inavutia upande wake.

Cha kutupa moyo ni kwamba, kwakuwa Kenya na Uganda hazina tena washiriki kwenye BBA, huenda wakawa upande wetu, japo nalo si la kutegemea sana kwakuwa wenzetu wakati mwingine huamua kutupiga chini.

Uhusiano wake na Oneal ni advatange nyingine kwakuwa kama akiingia kwenye eviction, ni rahisi kwa Botswana kumwokoa shemeji yao. Ukiunganisha na kura za Kenya, Uganda, Tanzania na nchi nyingine zinazompenda Feza, huenda mambo yakawa mazuri kwake.

Kwakuwa shindano limebakiza wiki chache tu lifikie fainali, hofu kubwa imeendelea kutanda kwa washiriki wote wanaoombea kufika tu kwenye fainali na mengine Mungu ndio anajua.

Kuna watu wana wasiwasi kuwa Feza amekuwa mlaini sana na badala ya kujidhatiti kwenye The Chase, amekuwa mtu aliyetekwa zaidi na mahaba yake kwa Oneal, jambo ambalo wanahisi linaweza likamharibia, japo kwangu sioni kama ni tatizo. Kuna tatizo kwani kumpenda mtu?

Unadhani Feza Kessy anaweza kufika fainali? Maoni yako!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents