Habari

Fursa: Ray C atangaza ajira kupitia taasisi yake ya ‘Ray C Foundation’

Ray C Foundation iliyoanzishwa na msanii Rehema Chalamila aka Ray C mwaka huu kwaajili ya kutoa elimu kwa vijana na jamii juu ya madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya, sasa imetoa nafasi za kazi kwa watu wanaohitaji kufanya nae kazi.

RAY C F

Ray C ametangaza fursa hiyo kupitia Instagram:

“Ray C inatangaza nafasi za kazi zifuatazo….
1.Financial Manager. 2.Human Resource Manager 3.Secretary. Muombaji awe na Advanced Diploma au zaid katika nafasi anayo omba.Sifa nyingine awe anajua kusoma ,Kuandika na Kuongea vizuri Kingereza. Barua zote zitumwe kwa Email [email protected] Barua zote ziambatanishwe na vielelezo vyote muhimu Juu ya Elimu ya mwombaji,uzoefu wa kazi anayoiomba pamoja na mawasiliano hai.Aidha mwombaji aandike kwenye Kurasa inayojitegemea utayari wake wa kufanya kazi na Ray C Foundation katika mazingira tofauti na uzoefu wake wa kufanya kazi na NGOs (Kama anao).Watakaochaguliwa wataitwa kwenye usaili kwa email au simu(hakikisha unaandika namba yako ya simu).”

Ray C pia leo (May 15) anasheherekea siku yake ya kuzaliwa, na huu ndio ujumbe aliouandika katika siku hii muhimu kwake.

“It’s my Birthday people………Happy Born day to Mememememememeeeeeeeee !!!!!15th May,Nilizaliwa Siku Kama ya Leo!!!!!!hakuna ninachotaka kubadilisha kwenye Maisha yangu zaid ya kumshukuru Mungu kwa baraka zote alizonipa na kila Siku anaendelea kunifungulia Milango ya Neema !!!Thank You Jesus For everything!!!!”

Tunakutakia birthday njema Ray C.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents