Burudani

GK: Wasanii warudi shule ili waache kupelekwa pelekwa

King Crazy GK amewataka wasanii warudi shule ili waache kuendeshwa kwenye muziki.

jumaclick-blog-1

Rapper huyo amedai kuwa wasanii wengi wamekuwa wakipelekwa pelekwa na watu lakini kama wangekuwa na elimu wangeweza kujiamulia wenyewe cha kufanya.

“Wasanii warudi shule, wengi wamekuwa wakipelekwa pelekwa kwa kuwa hawana elimu. Kama ukiwa na elimu yako unaweza ukajiamulia mwenyewe cha kufanya kutokana na elimu uliyokuwa nayo na kikawa kizuri zaidi,” amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa TV.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mzuri Pesa’ ameongeza kuwa amekuwa akiwatumia madirector kutoka nje kwa kuwa wakija wanajua huku tunataka nini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents