Burudani

Haya ndio yaliyowapeleka Young Dee na Nyandu Toz Afrika Kusini

Kama unawa-follow Young Dee na Nyandu Toz utakuwa umekutana na post zao nyingi kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii zinazooonesha wako Afrika kusini.

N-Y

Haikuwa imewekwa wazi sababu zilizowapeleka huko, japo kutokana na ongezeko la wasanii wengi wa Bongo kwenda kufanya video Afrika Kusini, wengi walihisi pia na wao ndicho kilichowapeleka.

Young D na Nyandu wamesema kuwa wameenda Afrika Kusini kufanya show. “Nipo hapa na Nyandu Toz maeneo ya Johannesburg kwaajili ya maandalizi ya show yetu ambayo tutaifanya Pretoria terehe 7 Jumamosi mwezi huu wa 11.” Young D aliiambia 255 ya XXL.

Nyandu SA

“Kikubwa ni hicho ndo kimetuleta huku kwasababu tumeamua kuufunga mwaka kwa style ya tofauti kidogo kwasababu sehemu kubwa ya Tanzania tumeshaimaliza, na tukaona kuna mashabiki zetu wengi sana huku ambao hawajawahi kuniona na hawajawahi kupata bahati ya kuona performance yangu.” Alisema Young Daresalaam.

Mbali na show hiyo, rapper huyo amesema kuna kitu kingine kikubwa ambacho kimewapeleka; “Na ukiacha hivyo kuna mipango mingine kibao ambayo tutawapa taarifa as long as mtakuwa karibu na sisi na tutawajulisha kingine ambacho kitatokea pande hizi”. Alimaliza Young Dee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents