Burudani

Wema Sepetu ataja sababu za kufanya Movie yake na wasanii wa Ghana bila kumshirikisha msanii yeyote wa Kitanzania (Video)

Wema Sepetu ataja sababu za kufanya Movie yake na wasanii wa Ghana bila kumshirikisha msanii yeyote wa Kitanzania (Video)

Msanii wa Bongo movie pia aliyekuwa miss Tanzania 2006 Wema Sepetu amefunguka mwanzo mwisho kuhusu sanaa nzima ya Bongo movie. Msanii aliongea hayo wakati anaongea na waandishi wa habari juu ya movie yake ya D.A.D ambaye aliamua kwenda kuifanyia nchini Ghana na msanii kutoka nchini humo ambaye ni Van Vicker.

Wema alisema ” Niliamua kwenda kufanya muvi huko ili kubadilisha mazingira kidogo ya uigizaji kwani kama movie za Kitanzania na Kiswahili tulishafanya sana” aliongeza “Mimi ndio niliyemtafuta Van Vicker ili tufanye kazi lakini pia nilimwambia atafute waigizaji yeye mwenyewe anaona wanafaa”

Lakini pia alipoulizwa kuhusiana na tofauti iliyopo kati ya mazingira ya uigizaji ya Kitanzania na ya nchini Ghana alisema ” Mazingira ya wenzetu ni mazuri sana kwani wenzetu kila kitu wanachohitaji katika uigizaji wanapewa na serikali yao mfano wakitaka kuigiza hata Mahakamani wanapewa ruhusa ya kufanyia humo hata wakihitaji beki au hata uwanja wa ndege serikali yao inawasaidia tofauti na Tanzania mfano ukihitaji kuigiza katika uwanja wa ndege wanakwambia ufanyie nje na sio ndani sasa tasnia yetu haiwezi kuendelea kwaweli”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents