Habari

Hussein Machozi alia na waandaaji wa tuzo za Kili kwa kuipotezea ‘Addicted’ kwenye nominations

Tukiwa tunakaribia kuifikia siku ya tuzo za muziki Tanzania KTMA (June 8), mwimbaji wa Tanzania mwenye sauti ya kipekee Hussein Machozi ameonekana kusikitishwa kwa wimbo wake wa “Addicted” kutoingizwa katika tuzo hizo huku akiamini ni wimbo mzuri unaostahili kutokana na kufanya vizuri mwaka jana.

machozi7

Machozi ameiambia Bongo5 kuwa anasikitishwa sana na utaratibu uliopo kwa upande wa waandaaji kwa kushindwa kuzipa nafasi nyimbo zinazostahili kuingizwa katika tuzo hizo ikiwa ni pamoja na wimbo wake wa Addicted.

“Ukizungumzia ngoma 5 zilizofanya vizuri mwaka jana huwezi kuacha kuitaja Addicted, unajua Addicted imetoka June na mpaka mwezi wa 8 hivi ndo ikawa imeshika, lakini kuna nyimbo zimekuja kutoka baada yake lakini zimeingia, msanii kama Ally Nipishe alikuja kutoa wimbo wake Addicted ikiwa tayari iko juu lakini yeye na wengine wameingizwa. Mi naona hizi tuzo hazijakaa sawa na sizihitaji, siwezi kuhitaji kitu ambacho hakijakaa sawa ila naongea ili kuwaelimisha watanzania wanaonipenda wasife moyo kwa sababu mtu wao kutoingizwa kwenye hizo tuzo wasidhani kuwa sistahili. Video ya Addicted imechezwa kwenye vituo vikubwa kama Trace ya Ufaransa, Channel O na MTV za South Africa na kuna channel zingine za Nigeria kuna watu waliniambia kuwa huwa inachezwa, “alisisitiza Hussein.

“Kuthibitisha hayo mi nimewahi kupata tuzo Kenya katika tuzo ya Nzumari, so unaweza kuona kama watu wa nje wanauona umuhimu wangu manake ni kwamba ninastahili, lakini sasa tuzo ya nyumbani ni muhimu zaidi kwangu sababu hata kimataifa huwezi kupewa tuzo za kimataifa kama kwenye historia yako huna tuzo za nyumbani huwa ni ngumu japo Kenya wananithamini kama mtu wa kwao.”

Msanii mwingine aliyetoa yake ya moyoni kuhusiana na kutoridhishwa na nomination za KTMA kwa mwaka huu ni Khalid Mohamed a.k.a T.I.D ambaye (May 6) aliweka status katika ukurasa wake wa facebook inayosomeka: “Nashangaa kili awards kuniita then hawajaniweka hata kidogo hii maana nini au ndo roho mbaya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents