Burudani

Idris Sultan aachiwa kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa wiki moja

Mchekeshaji Idris Sultan na mwenzake Innocent Maiga wamesomewa mashitaka mawili katika Mahakama ya Kisutu ikiwemo kushindwa kufanya usajili wa simu kadi iliyokuwa inamilikiwa na Mtu mwingine, kosa hili linamkabili Idris, ambapo inadaiwa alitumia kadi ya simu iliyomilikiwa na Innocent Maiga bila kuripoti kwa mtoa leseni.

Mahakama ya Kisutu imesema kosa jingine ni kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya kadi ya simu linamkabili Innocent Maiga ambaye anadaiwa kuwa kinyume na sheria alishindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya namba ya simu kama inatumiwa na Idris Sultan.

Baada ya kusomewa mashitaka yao, Idris na mwenzake Maiga, wamekana makosa yao, ambapo upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili, waliosaini bondi ya Tsh. Mil 15 kila mmoja.

Wakili wa Idris, Benedict Ishabakaki ameondolewa kumuwakilisha Idris kwasababu atatumika kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kutokana na kushuhudia mshitakiwa wake akichukuliwa maelezo Polisi, hivyo anabakia Wakili Jebrah Kambole, kesi imeahirishwa hadi Juni 9, 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents