Habari

Injini mitumba za TRL kulipiwa bilioni 7/- kwa mwaka

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRL) jana lilipokea injini tisa mitumba kutoka India ambazo zitakodishwa kwa dola milioni sita (takribani Sh bilioni saba) kwa mwezi.

Evance Ng’ingo

 

 

 

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRL) jana lilipokea injini tisa mitumba kutoka India ambazo zitakodishwa kwa dola milioni sita (takribani Sh bilioni saba) kwa mwezi.

 

Sambamba na kuwasili kwa injini hizo zilizokwishatumika kwa miaka 10, mwekezaji katika shirika hilo, Ms Rites ya India imeahidi kuboresha huduma zake, ikiwa ni pamoja na kumaliza ukarabati na kufufua njia mpya baada ya kipindi cha miaka mitatu ijayo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya TRL muda mfupi kabla ya kushushwa kwa injini hizo zitakazotumika mahsusi kuvuta mabehewa ya mizigo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Narasimhaswami Jayaram alisema kuwa bado wanahitaji injini nyingine 20 kuweza kuboresha huduma hiyo kwa ukamilifu.

 

Jayaram aliongeza kuwa shirika hilo linatarajia kuanza kubeba mizigo ya hadi tani milioni mbili kwa miaka mitatu ijayo na hivi sasa wana uwezo wa kubeba tani 700,000 tu.

 

Aliongeza kuwa tatizo hilo linatokana na uchakavu wa reli ambako njia za reli ni za zamani ikilinganishwa na njia zinazotumika katika nchi nyingine. Mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, Siraju Kaboyonga alisema katika kipindi hicho cha miaka mitatu wanatarajia kufufua upya njia ya kwenda Tanga kuweza kumudu mahitaji wa wakazi wa huko.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents