Afya

Jinsi ya kutibu ugonjwa wa mafua

Mafua ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza hutokea mabadiliko ya kimwili ikiwemo sehemu za viungio vya mwili kama miguu, mikono na sehemu zingine.

Hizi ni baadhi ya njia za kawaida zinazoweza kusaidia kukutibu bila kiasili:

Ulaji wa machungwa

Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.


Inashauriwa kuwa ila unapokua machungwa basi hakikisha kuwa unakula na pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.

Maziwa ya Mtindi:

Unywaji wa maziwa ya mtindi ni moja ya njia inayosaidia kupunguza ugonjwa huo, hii ni kutokana na kuwa maziwa hayo yana kiwango kikubwa cha protini na mtu mwenye mafua hupunguza kukoha kwa kunywa maziwa hayo.

Asali na Tangawizi:

Asali ni dawa kubwa sana ya magonjwa mbalimbali, ila ukichanganya asali na tangawizi husaidia kutibu mafua na kifua, hii ni dawa nzuri sana kwani haina madhara yoyote unaweza kutumia kwa kuiramba ama kwa kuichanganya katika chai.

Chanzo: by Mitandao

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents