Burudani

Kalapina aeleza kilichompoteza Harmorapa

Msanii wa muziki wa rap Bongo, Kalapina amefichua kilichompoteza Harmorapa katika game baada ya kung’aa kwa kipindi kifupi.

Rapper huyo ambaye pia mtangazaji wa tv, amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm kuwa kupotea kwa Harmorapa kunatokana na kuwa kiki nyingi kuliko kazi.

“Kuna dogo mmoja alikuwa ana kiki alioneka hata wakati Mhe. Nape anatolewa kwaju katika mambo ya watu wasiojulikana yanaanza kurise akatoka baruti anaitwa nani yule mtoto? (Hamorapa), yeah!!, zilikuwa ni kiki kazi ndogo mcheki sasa yupo wapi” amesema Kalapina.

Amendelea kwa kusema kuwa kiki ni vitu vya uongo uongo na havina maana katika maisha ya kimuziki ya msanii badala yake wasanii wafanye kazi nzuri, waandike mistari ambayo inawashika watu mpaka mtu ajiulize huyo alifikiria nini kuandika hii ngoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents