Kama unashindana na sisi, unapoteza tu muda – P-Square
P-Square wamewaonya wasanii wa Nigeria na Afrika kwa ujumla wanaotaka kushindana nao kuwa wanapoteza tu muda.
Kauli hiyo wameitoa wakati ambapo Peter Okoye aliyeanzisha kipindi cha mashindano ya kucheza, Dance With Peter alipomwalika pacha wake Paul kama jaji mwalikwa. Walipata fursa ya kuulizwa maswali kadhaa ikiwemo mafanikio yao.
“Hatuna ushindani wowote; tunashindana sisi wenyewe. Kama unashindana na P-Square, unapoteza tu muda wako,” walisema.
Pia Paul alimsifia pacha wake kwa kuanzisha shindano hilo.
“I’m proud of this dude (Peter). When he brought up this idea of Dance With Peter, I doubted initially, but he stuck to his guns, and look at where we are now,” alisema.
Awali Peter alidai kuwa Paul naye atakuja na shindano lake la kuimba, Sing With Paul.