Burudani

Kampuni ya Dr. Dre yawafungulia mashitaka Wachina waliotengeneza faida ya $135 Billion kwa kuuza headphone feki za ‘Beats’

Kampuni ya Beats Electronics watengenezaji wa headphones maarufu za ‘Beats By Dre’ inayomilikiwa na producer mkongwe Dr. Dre, imeamua kuwachukulia hatua Wachina wanaoingiza mabilioni ya dola kwa kutengeneza na kuuza kwa bei ndogo headphone feki za Beats.

dre-e1399586836803

Kwa mujibu wa TMZ wachina hao wametengeneza faida ya dola bilioni 135 kwa kuuza headphone bandia kupitia website zao.

Kesi ya madai iliyofunguliwa na kampuni ya Dre inahitaji wachina hao kusitisha uuzaji wa headphone hizo na kunyang’anywa domain za website hizo.

Taarifa ya TMZ imeongeza kuwa Beats Electronics inahitaji kulipwa fidia ya faida iliyopatikana kutoka kwenye mauzo ya bidhaa hizo bandia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents