Michezo

Kichapo cha 5~1 chamshangaza Poulsen

jan_Poulsen2

Kichapo cha Taifa Stars cha 5~1 dhidi ya timu ya taifa ya Misri jana kimewastaajabisha wadau wengi wa soka nchini akiwemo kocha mkuu wa timu hiyo Jan Poulsen.

 

Akizungumza mapema leo kocha huyo amekiri kuwepo kwa makosa mengi kiuchezaji ambayo stars waliionyesha katika kipindi cha kwanza katika uwanja wa Arab Contractors.”Ninaamini stars walikuwa na kila sababu ya kuepukana na makosa waliyoyaonyesha lakini pamoja na hayo Misri imeonyesha ni timu yenye uwezo zaidi na stars wanahitaji juda tu wa kuyafanyia kazi mapungufu yao ili wawe katika kiwango kinchostahili.”

Mabingwa hao wa CECAFA Challenge Cup wamekiri kufanya vibaya kutokana na hali ya hewa kuwa baridi sana huko Misri, kwa mujibu wa nahodha wa stars Njasigwa Shadrack.

“Tunawasihi mashabiki wetu kutokata tamaa na sisi kwani tunazidi kujifua ili tuzidi kuwa stadi zaidi katika soka hasa dhidi ya wachezaji wenzetu wa nchi za Afrika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents