Habari

Mchafuko Jijini Arusha

maandamano2

Kwa kile kinachosemekana kuwa ni mchafuko ambao haujawahi kutokea, Jiji la Arusha jana limeshuhudia vita kati ya waandamanaji kutoka kwenye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Jeshi la polisi la taifa.

Inasadikika kwamba fujo hizo zilianza pale ambapo wanachama wa Chadema walisitishwa na jeshi la polisi kuendelea na maandamano hayo kwa kile walichokieleza kuwa ni tishio kwa amani mjini hapo.

Baada ya kutoelewana, viongozi wa CHADEMA waliwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Viongozi wa Chadema Waliotiwa mbaroni ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe,katibu mkuu wa chama hicho,Dr. Wilbroad Slaa,Mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema pamoja na mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mh Philemon Ndesamburo.

Serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha, imetoa taarifa kwamba watu wawili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa na kwamba wameamua kutatua tatizo hilo kwa njia ya maziungumzo.

Mh. Nahodha aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam akiwa na IGP Said Mwema, ambapo aliwahakikishia amani wakazi wa Arusha kwa kuahidi kutatua matatizo hayo yaliyosababisha mchafuko jana.

IGP Mwema amekiri kutoruhusu maandamano lakini kuruhusu mkutano wa hadhara kwa wanamchama hao, na hivyo kudai kukiuka kwao kwa sheria na tamko lililotolewa.

B5 iko mbioni kuongea na msemaji wa Chadema na itazidi kukuhabarisha yatakayojiri na sakata hili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents