Michezo

Leroy Sane hana mpango na Manchester City – Pep Guardiola

Kocha Pep Guardiola amesema kuwa nyota wake Leroy Sane amekataa ofa ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu ya Manchester City.

Pep Guardiola 'Not Involved' in Leroy Sane Transfer Talks Amid ...

Leroy Sane anaweza kuondoka dirisha hili baada ya kukataa kuongeza kandarasi ya kuendelea kusalia Manchester City.

City kwa muda sasa imekuwa ikiweka ofa mezani kwaajili ya kutaka kumbakiza mchezaji wake,  Sane lakini Mjerumani huyo ameonyesha nia yake ya kutaka kujiunga Bayern Munich.

Sasa Guardiola amethibitisha kuwa, Sane ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa hatosaini kandarasi mpya akimaanisha ataondoka pengine majira haya au yajayo ya joto.

Pep Guardiola confirms Leroy Sane will leave Man City at end of ...

Sane mweye umri wa miaka 24, atakuwa nje ya mkataba msimu ujao wa majira ya joto mwaka 2021 hivyo City italazimika kumuuza kwenye dirisha lijalo la usajili.1.

Akiongea kuelekea katika mchezo wao ujao kati ya City dhidi ya Burnley, Guardiola amesema “Leroy amesema hataki kuongeza kandarasi yake zaidi, hivyo anataka kuondoka.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents