Picha

Lulu aandika ujumbe wa kwanza kuhusu Kanumba ‘ulikuwa zaidi ya baba,kaka,mpenzi,mume’

Wakati zikiwa zimebaki wiki chache tu hadi kifo cha Stephen Kanumba kitimize mwaka mmoja, aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael aka Lulu kwa mara ya kwanza leo ameandika ujumbe kuhusiana na jinsi anavyomkumbuka.

Lulu-331

Lulu aliachiwa kwa dhamana mwezi January mwaka huu baada ya kukaa mahabusu kwa takriban miezi minane kufuatia kukamatwa kwa kuhusika na kifo cha Kanumba.

Lulu ambaye hivi karibuni amekuwa akitweet mara kwa mara ameandika:

“Ulikuwa zaidi ya baba,kaka,mpenzi,mume,ndugu,rafiki….sitoacha kukulilia katika maisha yangu yote!!R.I.P daddy angu STEVEN KANUMBA.”

Akiambatanisha na picha ya Kanumba, Lulu ameongeza, “I will alwayz love u daddy angu!”

Unaweza kumfollow Elizabeth Michael ‏Twitter kwa jina la @hotlulumichael.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents