Burudani

M2 The P awachana wasanii wanaoendekeza kiki

Msanii wa muziki Bongo, M2 The P amewatolewa uvivu wasanii wanaondekeza kiki hadi kusahau kufanya muziki wao.

M2 The P ameseme iwapo msanii anafanya hivyo awe na kazi nzuri zinazoeleweka na siyo kiki tu wakati hata kazi zake hazionekani.

“Kwangu kiki hazina umuhimu sana cha muhimu ni kufanya kitu kizuri, kiki zinakuja tu baadae, siwezi nikafanya kiki mwishoe ikaja kuniletea matatizo lakini ukifanya kitu kizuri kwenye muziki mzuri watu wataupokea tu,” M2 The ameiambia Bongo5.

“Kuna wasanii wameshakuwa katika mfumo ambao hawezi kutoa wimbo bila kiki, kiki nyingi halafu halfu mimi huwa sizifuatilii ni maneno tu ambayo huwa yanaongelewa mtaani na kupita” ameongeza.

Katika hatua nyingine M2 The P amesema yupo mbioni kutoa ngoma mpya baada ya ile ‘Nakuhonga’ ambayo alimshirikisha Mr. Blue iliyotoka miezi saba iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents