Burudani

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu AY – Part One – (Audio)

Jana July 5 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya AY. Jumatatu hii AY amezungumza na mtangazaji wa kipindi cha Chill na Sky, Fredrick ‘Skywalker’ Bundala na haya ni mambo 10 usiyoyajua kuhusu rapper huyo kutokana na mahojiano kwenye kipindi hicho.

AY

1. Yeye ndiye aliyemfanya TID aanze kuimba. TID alikuwa rapper na mshereheshaji (MC). Girlfriend wa CBM Crew ndio wimbo waa kwanza kwa TID kuingia studio. “Wakati TID ana host show nakumbuka wakati ule Casey alikuwa ametoa wimbo wake ‘Missing You’, so kwakuwa TID alikuwa ni rapper na alikuwa ana host shows, alikuwa anauchombeza ule wimbo. Nilikuwa nikimsikiliza nasema ‘huyu jamaa anajua kuimba kwahiyo nikaenda naye kwa Master J.”

2. Alizaliwa Shangani, Mtwara, July 5, 1982.

3. Ameishi kwenye mikoa mingi na Dodoma alikuwa akiishi mtaa mmoja na akina Mangwair. “Tumecheza wote, nilikuwa nawafundisha table tennis, roller-skates.”

4. Aliwahi kuingia fainali kwenye mashindano ya Umiseta kwa kucheza table tennis. Fainali zilifanyika Arusha.

5. Alianza kusoma darasa la kwanza kwenye shule ya Msingi Mwembeni ya Musoma, Mara. 6. Kundi lake la kwanza la hip hop liliitwa ‘Two Problem’ akiwa na Swedi na Aluta

7. Aliandaa show yake ya kwanza kama promoter akiwa kidato cha pili. “Niliandaa show nikawaleta GWM, wakati huo wanapiga ‘Cheza Mbali na Kasheshe’, halafu unawatoa watu Dar unawaleta Dodoma, unawalipia nauli nini, nakumbuka alikuja KR na Inspekta Haroun.”

8. Wimbo wake wa kwanza kuingia studio unaitwa Kipi Kikusikitishacho

9. Alihamia kutoka Morogoro kuja Dar kutafuta maisha na hakuwa na ndugu. “Nilikuwa nakaa kwa washkaji, nilikuwa nakaa kwa akina Buff G na kwingine. Chumba changu cha kwanza kupanga kilikuwa Magomeni.

10. TV yake ya kwanza kuinunua bado ipo. “Mpaka leo inawaka, haijawahi kuharibika hadi leo.” Chanzo: Chill na Sky.

Sikiliza kipindi hicho hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents