Burudani

Maua Sama ajiandaa kufanya video ya ‘Let Them Know’

Muimbaji anayefanya vizuri kwenye muziki hapa Bongo kwa ngoma zake kama ‘So Crazy’ na ‘Let Them Know’, Maua Sama ambaye anaishi, Moshi mkoani Kilimanjaro, amesema yuko mbioni kufanya video ya ‘Let Them Know’.

Maua-Sama
Maua sama

Maua Sama alikuwa akiongea na Bongo5 mjini Moshi na kueleza pia kwanini nyimbo zake hazijahit kama So Crazy.

” Unajua mashabiki wangu naona wananilielewa zaidi katika muziki wa RnB ila unajua muziki ni feeling kwahiyo unakuta inakuja feeling hiyo hiyo unajikuta unafanya hicho hicho kwahiyo wasijali mashabiki wangu kuna ngoma zinakuja watafurahia nina imani. Pia unajua watu wengi wamekuwa wakiniuliza kuhusu kufanya video tatizo unakuta muda wangu wa masomo unakuwa unaingiliana na muda wa muziki. Unajua masomo ni muhimu sana lakini hivi karibuni ntakuwa nipo free kwahiyo ntaenda Dar kufanya video ya wimbo wa ‘Let Them Know’ . Pia kuna ngoma zingine naenda kurekodi na nitakuwa na project nyingine na pia nafurahi kupata nafasi kufanya show katika tamasha kubwa kama hili la Serengeti Fiesta, ukizingatia nitakuwa home kwahiyo mashabiki wangu watafurahia show.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents