Burudani

MB Dog kuja na documentary ya maisha yake ya muziki

MB Dog amesema anajipanga kuachia documendary itakayokuwa inazungumzia maisha yake ya muziki.

mbdog

Muimbaji huyo aliyewahi kuhit na ngoma kama ‘Latifa’ na ‘Si Uliniambia’ amesema ameamua kuachia documentary hiyo baada ya kuona mashabiki wanahitaji.

“Awali kidogo Desso alifanya kama movie yake fulani hivi kwahiyo alifanya kama kunishirikisha ‘bwana njoo unipe support’, sasa kile kitu kikawa kimeniletea shida sana kwa raia wengi, kutoka Rwanda na Burundi. Napokea simu kutoka sehemu nyingi na kila nikipigiwa simu watu wanazungumzia hiyo kitu. Ndioa nikaona nitumie nafasi hii kutengeneza documentary,” amesema muimbaji huyo.

“Natumaini watu wanataipenda na wataiangalia. Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinadadavua kuhusu maisha fulani ambayo niliyapitia na tayari imeshakamilika na ipo katika kiwango kimoja kizuri ili wale waliokuwa wanasumbuka na kile kipande kidogo nilichokafanya waangalie hii,” MB Dog aliiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM.

Ameongeza kuwa documentary hiyo imeandaliwa katika miji mbalimbali ambapo pia Q Chief ataonekana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents