Michezo

Mourinho: Sina huruma na West Ham United

kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa hana huruma na West Ham kufuatia ushindi wa 2-0 timu yake ilioupata katika uwanja wa London siku ya Jumatatu.

West Ham walimaliza mchezo vibaya huku wakiwa pungufu baada ya mwamuzi Mike Riley, ambaye alimtoa kwa kadi nyekundu Sofiane Feghouli baada ya dakika 15 tu kabla ya Zlatan Ibrahimovic kufunga goli ambalo alikuwa ameotea.

Mourinho amelalamika kuwa timu yake ilifanyiwa makosa mengi ya maamuzi kwani hakuwa akifurahishwa na maamuzi ya waamuzi tangu mwanzo wa kampeni za msimu huu.

“Sina huruma na West Ham – Siangalii maamuzi. Nadhani iwapo utazungumzia maamuzi, sisi ndio mabingwa wa maamuzi mabaya,” aliambia BBC Sport.

Mourinho pia aliambia Sky Sports News: “Sikufanya lolote kwa ajili ya kadi ile nyekundu. Nilikuwa mbali sana na sikuiangalia hata kwenye runinga.

“Nimelazimika kujielimisha binafsi tangu mwanzo wa msimu kwa sababu ya maamuzi mengi sana mabaya – Goli la Zlatan lililokataliwa, penalti ya wazi dhidi ya Crystal Palace. Ulikuwa wakati mgumu sana kwetu, kwangu zaidi.”

Ushindi huo unafanya Manchester United ibakishe pointi moja kuifika timu ya nne kwenye msimamo.

Source: Goal.com

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents