Burudani

Msanii wa Nigeria, Tekno akanusha kuwahi ‘kutembea’ na Masogange

Msanii wa Nigeria anayehit na wimbo wake uitwao Duro amekanusha kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na Agnes Masogange.

maso

Miezi kadhaa iliyopita ziliwahi kuwepo tetesi kuwa msanii huyo ni mmoja wa wanaume waliofaidi umbo la video vixen huyo mwenye umbo la utata.

12105083_509754609200284_1777610319_n

Masogange aliwahi kupost mfululizo wa picha za Tekno kwenye Instagram kuonesha mahaba mazito kwake, hali iliyozusha tetesi kuwa wawili hao ni ‘item.’

Akiongea na Diva wa Clouds FM kwenye kipindi cha Ala za Roho, Tekno alisema yeye na Agnes ni washkaji tu.

“I never had sex with Agnes,” alisema Tekno.

Amedai kuwa urafiki wao ulikuwa wa Instagram zaidi na pamoja na kuwa walikutana nchini Nigeria hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents