Burudani

Rihanna asema akipata nafasi ya kuja tena Afrika itakuwa ni kwaajili ya show ya bure!

Katika mahojiano na jarida la The New York Style, mwimbaji wa Barbados, Rihanna amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kuja tena Afrika basi huenda ikawa ni kwaajili ya kufanya show ya bure.

Riri

Bahati mbaya ni kuwa hii haiwahusu mashabiki wa Afrika Mashariki kwasababu staa huyo alikuwa akizungumzia Afrika Magharibi.

“You know what? If I ever go to West Africa, it would probably be for a free concert. I would want to do something for the people there. Maybe we can make a whole event; the way Bob Marley would have done it. Just for the people. And if they climb over the gate, let them climb over the gate.”

Riri ambaye anatarajia kuachia album yake mpya ‘ANTI’ mwaka huu, amewahi kutumbuiza Johannesburg na Cape Town, Afrika Kusini mwaka juzi 2013 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya ‘Diamonds World Tour’, na mwaka huo huo alitumbuiza Morocco kwenye tamasha la Mawazine. Hajawai kuja Afrika Mashariki wala magharibi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents