Burudani

Mtoto wa Jackie Chan, Jaycee afungwa jela miezi 6 kwa kosa la kuvuta bangi

Mtoto wa Jackie Chan, Jaycee Chan amefungwa jela miezi sita kutokana na kosa la matumizi ya bangi. Amepigwa pia faini ya $322.

Jessica-Cambensy-and-Jaycee-Chan-in-Double-Trouble-2012-Movie-Image

Chan, 32, alipatikana na hatia kwenye mahakama ya Beijing nchini China kwa kuwahifadhi wengine nyumbani kwake kutumia madawa.

Polisi walivamia nyumbani kwake na kukutana gram 100 za bangi.

Jackie Chan aliyewahi kuwa balozi wa kitengo cha polisi cha kuzuia madawa ya kulevya alidai kuwa mwanae amemuabisha na alisikitishwa na tabia yake.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents