Burudani

Muziki wangu utapita katikati ya Diamond na Alikiba – Z Anto

Msanii wa muziki, Z Anto amedai hana sababu ya kupitia njia ambazo wanapita wasanii Diamond na Alikiba ambao wanaangaliwa zaidi kwa sasa.

Z Anto ambaye amewahi kuwika na wimbo kama ‘Binti Kiziwi’, ameimbia Bongo5 kuwa ametafuta njia ya kutoboa katika muziki wake bila kufanya aina ya muziki ambao wanafanya wakali hao wawili.

“Mimi ni mkongwe kwenye huu muziki na bado nina nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi,” alisema Z Anto. “Najua kwa sasa Diamond na Alikiba ndio wasanii wanaozungumziwa zaidi lakini mimi sina haja ya kushanda nao muziki wangu nitaupitisha katikati yao,”

Muimbaji huyo ambaye pia ni mfanyabishara amedai kwa sasa anakuja na management yake mpya ambayo itaikabidhi jukumu la kuusimamia muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents