Burudani

Mwana FA atoa sababu za kwanini haupendi muziki wa kina Davido, P-Square na Wanaija wengine

Pamoja na jitihada za baadhi ya wasanii wa Bongo kufuata nyayo za muziki wa Naija katika nyimbo zao kwa kuamini kuwa ndio zinazokubalika zaidi sokoni kwa sasa, rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema hapendi kusikiliza muziki wa Nigeria na ametoa sababu za kuwa hater wa kazi za kina Davido, Wiz Kid, P-Square na wengine.

BINAMU

F.A alitweet, ‘katika habari nyingine,nimeamua kuwa hater wa mziki wa Nigeria..’.

Haya ndio maelezo ya kwanini ameamua kuwa hater wa muziki huo licha la kumshirikisha J. Martinz wa Naija katika duet yake na Ay ‘Bila Kukunja Goti’ mwaka jana.

“Mimi nikisikiliza muziki wa Nigeria hata nikisikiliza ufundi wao jinsi wanavyoimba sioni kama jamaa wanakuwa mafundi hivyo” alisema Binamu kupitia 255 ya XXL.

“Naamini tuna watu wengi ambao wanaimba vizuri zaidi yao hapa lakini kwasababu watu wanafanya double standards wanauangalia muziki wa Nigeria kivingine na muziki wa kibongo kivingine inakuwa shida”.

Ameendelea kusema,
“Ukimweka mtu kama Ben Pol utapata shida sana kutafuta mwanamuziki wa Nigeria ambaye anaweza kumatch naye kwa uwezo wa kuimba.”

FA ameongeza kuwa kinachowasaidia Wanaija ni vile walivyoamua kuupa nafasi muziki wao zaidi ya muziki kutoka sehemu nyingine ndio sababu nyimbo zao zinapenya kirahisi.

“Wameamua tunataka kuunga mkono muziki wetu na muziki wao ndo unapigwa sana usiniambie kwamba wanaamini kwamba muziki wao ndio muziki mzuri kuliko yote duniani, lakini ni kwasababu wameamua sisi tuna shutdown watu wote wengine tuna support muziki wetu tu.”

Binamu ametoa ushauri wa ku-support muziki wa nyumbani zaidi kwa kutolea mfano wa Afrika Kusini wanavyoupa zaidi nafasi muziki wao zaidi ya ule wa Naija tofauti na ilivyo bongo.

“Kwa mfano kwenye Channel O Music Awards…Wasouth Afrika wanamatatizo kabisa na Wanaijeria, kwa mfano utakuta katika category 20 hivi ambazo zipo, Wanaigeria wakipata sana wanapata nne, na hata uwezo wa kupiga show wa Wanaigeria South Afrika hauko, yaani hamna show ile kama sijui D’Banj amekuja sijui Davido amekuja hapa, jamaa hawawapi hizo show, wanasema kwasababu jamaa wana support muziki wao peke yao hawataki ku-support mtu mwingine yeyote we must as well support our music tukaachana na hiyo habari.”

Ushauri wa Binamu kwa wapenda burudani wote wa nyumbani:

“Ifike mahali tusupport muziki wetu tusupport watu wetu tuone kama tunaweza kupiga hatua.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents