Burudani

Nahreel aeleza maana ya ‘Above In A Minute’ ambayo husikika kwenye nyimbo za Navy Kenzo

Ukisikiliza baadhi ya nyimbo za kundi la Navy Kenzo ikiwemo ‘Game’ kuna maneno wanapenda kuyasema, “Above In A Minute”, lakini inawezekana hujui ni kwasababu gani wanapenda kuyatumia au yana maana gani kwao.

Nahreel

Mbali na nyimbo, hata post zao za mitandao ya kijamii, Nahreel na aika huwa wanaweka hashtag ya #AboveInAMinute kwenye post zao nyingi.

Mwimbaji wa Navy Kenzo ambaye pia ni producer wa The Industry, Emmanuel Mkono maarufu kama Nahreel amesema kuwa “ABOVE IN A MINUTE” ni jina la album yao mpya ambayo bado iko jikoni.

Akizungumza kwenye kipindi cha MKASI kupitia EATV, Nahreel amesema maneno hayo waliyachukua kwenye moja ya mistari ya Aika kwenye moja ya nyimbo zao na kuamua kufanya liwe jina la album yao.

Navy Kenzo kwa sasa wanafanya vizuri kwenye chati za vituo mbalimbali vya TV na Radio Afrika kupitia hit yao ya ‘Game’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents