Michezo

Namungo FC watinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika

Wauaji wa Kusini, Namungo FC wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya ushindi wa jumla wa magoli 7-5.

Namungo FC imemaliza dakika 90 kwa kufungwa goli 3 – 1 dhidi ya CD de Agosto (Agg. 7-5). Wakiwa na msimu wa kwanza katika michuano ya Kimataifa wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi hakika wanastahili pongezi.

Katika hatua ya makundi ya Michuano hiyo Namungo FC Inayonafasi ya kusajili jumla ya wachezaji 10 wapya kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika CAF.

Namungo FC sasa inajiunga katika kundi D, lenye timu za Raja Casablanka ya Morocco,🇲🇦 Pyramidis ya Misri,🇪🇬 na Nkana ya Zambia,🇿🇲.

Hongera @namungofc kwa kufanikiwa kuingia hatua hiyo ya makundi Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents