Burudani

Ne-Yo afunga ndoa na mchumba wake Crystal Renay

Muimbaji wa R&B, Ne-Yo amefunga ndoa na mchumba wake Crystal Renay.

ne-yo-1024

Harusi yao ilifungwa Jumamosi mbele ya wana familia na marafiki huko Rancho Palos Verdes, Los Angeles, Marekani.

“Tuna hamu ya kuanza maisha pamoja,” Ne-Yo aliliambia jarida la People. “Tunatarajia kuwa marafiki wa dhati.”

Wamefunga ndoa wakati ambapo wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

Ne-Yo tayari ana watoto wawili, wa kike Madilyn Grace, 5, na wa kiume Mason Evan, 4 kutoka kwenye uhusiano wa zamani.

Muimbaji huyo anatarajiwa kutumbuiza jijini Mwanza, May 21.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents