Burudani

Ne-Yo na mchumba wake wafunga ndoa na wanatarajia kupata mtoto

Superstar wa Marekani ambaye siku chache zilizopita alikuja Afrika Mashariki kwenye Coke Studio Africa, Ne-Yo amewa surprise mashabiki wake kwa mambo mawili makubwa kuhusu mahusiano yake.

Surprise ya kwanza ni kuwa Ne-yo tayari ni mme wa mtu, amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu aitwaye Crystal Renay.

Kama haitoshi, licha ya wawili hao kufunga ndoa lakini pia mke wake ni mjamzito na wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

crystal
“Surprise!!!!!”

Kupitia Instagram Ne-Yo amepost picha ya mke wake akiwa ameshika picha yao Ne-yo akiwa amesmhika tumbo na kuandika ‘Surprise!!!!!’.

neyo2
“Rest your soul chocolate, I’m watching over your heart now ? #neyo #CrystalRenay”-Crystal

Mke wake pia amepost picha yao na kuandika, “Rest your soul chocolate, I’m watching over your heart now ? #neyo #CrystalRenay”.

neyo3

Na katika picha ingine aliandika “No matter what they say” our Miracle is on the way and I couldn’t feel more blessed. You’re negativity means nothing to us. We are happy, we’ve BEEN happy and will always be HAPPY no matter what they say ? Thanking The Lord above for those who know my story know what this absolute miracle means to me. #BabySmith #Neyo #CrystalRenay #GodsChild #WasAlwaysInHisTime #BlindFaith ? thank you all who are happy for our happy photo by @kincordell”

Chanzo kimoja kimeithibitishia Entertainment Tonight kuwa Ne-Yo na Crystal wamefunga ndoa na wanatarajia kupata mtoto.

Ne-Yo tayari ana watoto wawili aliowapata na mke wake wa zamani Monyetta Shaw.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents