Michezo

Nilinunua jezi ya Simba ili niivae Vs Kaizer -Tarimba baada ya SportPesa kuwapa Simba Milioni 50 (+Video)

Kampuni ya burudani na michezo @tzsportpesa leo imekabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 50 kwa timu ya @simbasctanzania baada ya kufuzu hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya #CAFCL ikiwa ni bonasi kwa hatua waliyofikia.

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za SportPesa ambao ni wadhamini wakuu maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Waliohudhuria kutoka SportPesa ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, kutoka Simba SC ni Mkurugenzi Mtendaji Barbara Gonzalez, Msemaji Mkuu Haji Manara, benchi la Ufundi na baadhi ya wachezaji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Simba kwa hatua waliyofikia.

”Nawapongeza viongozi na wachezaji wa Simba SC kwani mmewapa heshima kubwa wana msimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi kama wadhamini wenu wakuu kwa mafanikio makubwa na kupambana mpaka kufikia hatua hii.”

”Hii ni ishara nzuri kwa mashindano yajayoo kwani mtashiriki kwa kujipanga ili kutimiza lengo lenu kama timu.”

Akiongea kwa upande wa Simba SC, Mkurugenzi Mtendaji Barbara Gonzalez alianza kwa kusema ” Kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Simba SC Mohammed Dewji napenda kuwashukuru SportPesa kwa moyo wao na kuendelea kutupa ushirikiano na kupelekea sisi kufika katika hatua hii.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents