BurudaniVideos

Niliugua vitu ambavyo si vya kueleweka sana – Tanzania (Video)

Tanzanite amedai kuwa ukimya wake ulisababishwa na mitihani ya dunia na kusumbuliwa na maradhi ambayo hayakuweza kupata ufumbuzi kwa dawa za kisayansi – translation, alirogwa.

“Mimi niliugua vitu ambavyo naweza kusema sio vya kueleweka sana,” ameiambia Bongo5.

“Kwa sisi ambao tunatokea kwenye familia za kawaida, nafikiri tutakuwa tumeelewana zaidi. Maradhi ambayo si ya kawaida ni yale maradhi ambayo unaweza ukaumwa na ukaenda hospitali ukaambia ‘mbona hauna tatizo.’ Lakini huku unatetemeka, yaani hali yako si nzuri labda jua kali wewe umevaa makoti matatu. Kuumwa nimeumwa, nisiwe muongo,” amesisitiza.

Japo hajasema aliwezaje kujiondoa kwenye mtego huo, anashukuru Mungu kuwa amerudi tena kwenye reli kuendelea na muziki na ameachia wimbo uitwao Usinipite.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents