Burudani

Nimeamua kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa wimbo mpya – Lady Jaydee

Msanii mkongwe wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amefunguka kwa kusema kuwa hataki tena kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia kazi.
Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Sawa na Wao’ hivi karibuni, amekiambia kipindi cha East Africa Breakfast kinachoruka East Africa Radio kuwa anachofanya ni kutoa kazi moja moja kutoka katika albamu yake mpya iitwayo’Women’.

“Unajua mimi nina marafiki mbalimbali wa rika zote, wapo walionizidi sana umri, wapo nalingana nao na wengine ni wadogo zangu kabisa hivyo muda mwingi napotoka nao au kujichanganya nao ndipo nikapata wazo la wimbo huu ‘Sawa na wao’ kwani binadamu tunatofautiana. Saizi nimeamua kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa kazi moja kutoka kwenye album yangu hiyo ya ‘Woman’,” alisema Lady Jaydee.

Lady Jaydee amesema wazo la wimbo ‘Sawa na Wao’ ambao ameuachia hivi karibuni alilipata kutokana na maisha ya watu wake wa karibu ambao amekuwa akiishi nao katika maisha ya kila siku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents