Burudani

One The Incredible ataja nani ni rapper, na nani MC kwenye hip hop ya Bongo (Audio)

Nini tofauti kati ya rapper na MC? Huo ni mjadala ambao haujawahi kuwa na mwisho. Wiki hii, One The Incredible aliulizwa kwenye kipindi cha Twenzetu cha Times FM kuhusu tofauti ya watu hao wawili.

“Rapper ni mtu yeyote tu anayeweza kuchana,” alisema One. “MC ni mtu ambaye anaweza kuchana kwa kutumia miundo mbinu au misingi ya sanaa ya kughani yenyewe kwamba mimi ninavyosema punchline sio kwamba ni mstari tu fulani wa ajabu ajabu ambao nimeuwaza nimeuweka kwenye mistari, hapana. Ni kitu ambacho ninapoandika kitu ili nitimize lengo au nitengeneze picha ya kile ninachokisema, ninajua kabisa technically, kuna kitu fulani nataka kukiweka hapa ili kujenga ile picha zaidi ya kutumia tu mstari ambao uko wazi,” alieleza One.

“Kwahiyo MC ni mtu ambaye yuko aware na kile anachofanya, anaulewa, na anakifanya kile kitu kwa malengo. Rapper ni mtu tu ambaye anajua kurap na hao wapo wengi tu, washkaji kibao ambao wanasimama hata mtaani hawana kazi wanarap. Kwahiyo marapa wako wengi, lakini MC kama MC ni watu wachache sana.”

Hapo ndipo mtangazaji wa show hiyo, One B (Moko Biashara), alipomuomba The Incredible amtajie majina halafu aseme iwapo msanii huyo ni rapper au MC.

Hivi ndivyo One aliwaelezea kila mmoja :

Yeye mwenyewe – MC
Nicki Mbishi – MC
Godzilla – (anajifikiria kwa muda) ni MC lakini sio katika definition yangu, ni MC pia sababu huwezi ukamweka Zilla katika group la marapa.

Joh Makini – Rapper
Roma – MC
Nick wa Pili – 50/50
G-Nako – Ni MC ila sijui sasa hivi ni nani,lakini mimi ninavyomjua G-Nako ni MC

Quick Rocka – Rapper

Madee – Rapper. Tena sasa hivi sijui hata bado ni rapper pia sababu hajarap muda mrefu. Ili uwe considered rapper uwe kwanza unarap. Sasa kama unaimba, katika nyimbo 10, nyimbo mbili ndio unarap siwezi kuconsider sababu Chris Brown pia anajua kurap lakini hatusemi ni rapper.

Mansu Li – MC
Fid Q – MC
Young Dee : Ni rapper asilimia kubwa zaidi ya MC, ana uwezo wa kuwa MC, kwamba ana uelewa wa kile anachokifanya lakini ameamua kufanya rap zaidi.

Dogo Janja – Rapper
Nyandu Tozi – 50/50
Mr Blue – ni mtu ambaye anajielewa lakini anaamua kurap, kwahiyo siwezi nikasema ni rapper lakini in a way vile vile siwezi nikaprove kwa watu kwamba ni MC kwasababu hatujawahi kufanya kitu.

Wakazi – MC
Profesa Jay – MC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents