Burudani

Papii Kocha na Babu Seya kuja na show yao ya kwanza ‘The Viking’s Night’

Mashabiki wa muziki nchini Tanzania pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla wanajipanga kushuhudia show ya kwanza ya kukata na shoka kutoka kwa Papii Kocha pamoja na Babu Seya ‘The Viking’s Night’ inayotarajia kufanyika March 10 mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es salaam.

Papii Kocha na Babu Seya

Itakuwa ni show ya aina yake ndani ya mwaka 2018 kutokana na wakongwe hao kutoonekana stejini kwa miaka mingi kutoka na kifungo.

Wawili hao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuwanajisi watoto 9 lakini baadaye waliachiwa kwa msamaha wa Rais Jonh Pombe Magufuli katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru baada ya kutumikia jela miaka 13 na miezi minne.

Mmoja kati ya wasanii hao, Papii Kocha ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Waambie’ ambao umeonekana kupenda na mashabiki wengi wa muziki nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents