Burudani

Picha: H.Baba na mkewe Flora Mvungi wapeana tuzo, sherehe zafana

Msanii wa muziki H.Baba akishirikiana na mke wake Flora Mvungi Jumamosi ndani ya Giraffe Ocean View Hotel wamefunga ukame wa tuzo kwa kupeana wenyewe kwa wenyewe baada ya kuona kila mmoja kati yao ana mchango kwenye muziki na filamu.

Rais wa shirikisho la wasanii Ado Novemba akimkabidhi tuzo ya msanii bora wa kutumbuiza H.Baba
Rais wa shirikisho la wasanii Ado Novemba akimkabidhi tuzo ya msanii bora wa kutumbuiza H.Baba

Tuzo hizo zinazotambulika kama ‘Tuzo za kifamilia’ zilihudhuriwa na rais wa shirikisho la filamu Tanzania, Simon Mwakifamba, rais wa shirikisho la muziki, Ado Novemba, wanafamilia mbalimbali pamoja na waandishi wa habari na zilifanyika kama tuzo zingine zilivyo.

Wengine walioibuka na tuzo ni Muongozaji mkongwe wa filamu Jully Tax pamoja na mtoto wa H.Baba ‘Tanzanite’.
Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba akimkabidhi tuzo Flora  Mvungi ya muigizaji bora wa kike
Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba akimkabidhi tuzo Flora Mvungi ya muigizaji bora wa kike

Akizungumza na wadau mbalimbali, H.Baba ambaye amepata tuzo ya mtumbuizaji bora wa muziki, alisema yeye ndio msanii anayestahili kupata tuzo kama hiyo kwa Tanzania.

H.Baba akizungumza huku akiwa ameshika tuzo yake
H.Baba akizungumza huku akiwa ameshika tuzo yake

“Tuzo hii hapa ni ya mtumbuizaji bora Tanzania,” alisema muimbaji huyo. “Mimi nina tuzo ya East Africa mtumbuizaji bora, Tanzania sina hata tuzo moja kwa sababu ya nini nimeshatangaza naanzisha hii tuzo kwa akili timamu na wala sivuti bangi. Mimi sivuti sigara wala sinywi pombe, kama kuna msanii anaona hii tuzo sio halali yangu mimi ajitokeze. Promota yoyote ajitokeze huyo msanii alipwe pesa mimi nita- perform bure na awadhihirishie watanzania kwamba yeye ni mkali ya stage Tanzania. Kama ananizidi mimi, promota amlipe yeye ila mimi kama H.Baba nitaperform bure na nitakuja peke yangu na yeye inatakiwa aje peke yake. Kwa sababu kuna Kiswahili fasaha ambacho kinakosewa kuna neno linaitwa mtumbuizaji bora na kuna watumbuizaji bora. Mimi ni mtumbuizaji bora, wengine ni watumbuizaji bora,” alijinadi H.Baba.

“Kwanini nasema watumbuizaji bora kwa sababu msanii yeye mwenyewe hajiwezi mpaka awe na watu wakucheza naye, ila mimi binafsi najiweza kwa sababu mimi mwenyewe ninaweza fanya kazi na ikaeleweka. Ndiyo maana ya hii tuzo niliyopata leo.”

“Ninaowatambua walikuwa watumbuizaji na ninawaheshimu mpaka leo nawataja watu wawili, kuna Mr Nice kuna TID (Top In Dar ) hao ndo watu wanaweza kusimama kwenye show na kuburudisha na watu wakasema asante,” alisema H.Baba.

Pia kwa upande wake rais wa shirikisho la filamu Tanzania, Simon Mwakifamba amempongeza H.Baba na mke wake kwa kuamua kupeana tuzo.

“Mimi nilivyosikia hili suala sikulielewa elewa lakini sasa hivi ndo nimeelewa nini maana ya hizi tuzo. Hii ni kupeana motisha ndani ya familia, kila mmoja ameona mchango wa mwenzake kwenye sanaa. H. Baba ni msanii wa muziki na Flora ni muigizaji kama wameamua kupeana tuzo mimi naona ni jambo jema,” alisema Mwakifamba.
Juli Tax akikabidhiwa tuzo na Kenneny
Jully Tax akikabidhiwa tuzo na Kenneny
H.Baba na mwanae Tanzanite
H.Baba na mwanae Tanzanite
Pokea zawadi mama Tanzanite
Pokea zawadi mama Tanzanite

Frola Mvungi akifurahia zawadi ya pesa kutoka kwa Mwakifamba
Flora Mvungi akifurahia zawadi ya pesa kutoka kwa Mwakifamba

H.Baba akikabidhi wa pesa kutoka kwa rais wa shirikisho la wasanii Ado
H.Baba akikabidhiwa pesa kutoka kwa rais wa shirikisho la wasanii Ado

Tanzanite akiwa ameshika pesa
Tanzanite akiwa ameshika pesa

IMG_5855

IMG_5875

IMG_5884

IMG_5897

IMG_5899

IMG_5902

IMG_5903

IMG_5920

IMG_5929

IMG_5942 - Copy

IMG_5945

IMG_5948

IMG_5963

IMG_5965 - Copy

IMG_5979

IMG_5983

IMG_5985

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents