Burudani

Picha: Iyanya alivyowasha moto kwenye Pool Party nchini Kenya

Wikiendi iiyopita msanii kutoka Nigeria, Iyanya alitumbuiza nchini Kenya katika sherehe za Pool Party zilizofanyika katika ukumbi wa B-Club ya mjini Nairobi.

Katika sherehe hiyo mkongwe wa muziki nchini humo, Nameless aliongoza kuwasha moto katika jukwaa hilo akiwemo na Iyanya, pamoja na wasanii wengine wa Uganda, Eddy Kenzo na Pallaso. Inadaiwa kuwa kiasi cha dola 100,000 kimetumika kuandaa sherehe hiyo pamoja na kuwakutanisha wasanii hao.

B Club imewahi kuwaalika wasanii kibao akiwemo Diamond, Venessa Mdee, Ommy Dimpoz, Darassa, Ben Pol, Dj Maphorisa, Seyi Shay,Trey Songz na wengine. Hizi ni baadhi ya picha katika sherehe hiyo ya Pool Party.

Imeandikwa na: Teddy Agwa
Facebook: Teddybway
Instagram: Tedbway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents