Burudani

Nafikiria kuachia albamu yangu na Belle 9 – G Nako

Wasanii wengi wa Bongo kwa sasa wamevutika zaidi na kuachia albamu – G Nako ni mmoja kati ya wasanii hao.

Rapper huyo ameweka wazi kuwa, kwa sasa anampango wa kuachia albamu yake aliyoshirikiana na Belle 9 ambayo itatoka kati ya mwezi Septemba au Oktoba mwaka huu.

“Albamu ambayo naishughulikia kwa sasa ni albamu yangu ambayo nitafanya na Belle 9, ndio ambayo ipo katika mpangilio wa kutoka na haitachelewa sana. Nafikiria kabla ya mwezi wa tisa au 10 itakuwa ipo tayari kabisa,” ameiambia Metro FM ya Mwanza.

Rapper huyo ameongeza kuwa wimbo wa ‘Ma Ole’ ambao ameshirikishwa na Belle utapatikana katika albamu yao hiyo. Kwa sasa G Nako ameachia wimbo wake mpya ‘Lucky Me’ ambapo ameahidi kuachia video yake hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents