Burudani

Picha: Mshindi wa milioni 60 za BSS 2015 kujulikana Ijumaa hii

Mashindano ya kusaka vipaji vya muziki nchini Tanzania kwa mara ya nane mfululizo, Bongo Star Search (BSS) yatafika tamati Ijumaa hii ambapo mshindi atajishindia shilingi milioni 60.

Jaji mkuu wa shindano la BSS 2015,  Madam Rita Paulsen
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Rita Paulsen

Washiriki walioingia 6 bora na wanaohitaji kura za wananchi ili kushinda ni Frida Amani BSS 106, Kayumba Juma BSS 116, Anger Mary BSS 106, Nassib Fonabo BSS 103, Jackline Kayengi BSS 118 pamoja na Kelvin Gerson BSS 110.

Washiriki walioingia top six, kuanzia kulia, Frida Amani BSS 106, Kayumba Juma BSS 116, Anger Mary BSS 106, Nassib Fonabo BSS 103, Jackline Kayengi BSS 118 pamoja na Kelvin Gerson BSS 110.
Washiriki walioingia top six, kuanzia kushoto, Frida Amani BSS 106, Kayumba Juma BSS 116, Anger Mary BSS 106, Nassib Fonabo BSS 103, Jackline Kayengi BSS 118 pamoja na Kelvin Gerson BSS 110

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, jaji mkuu wa shindano hilo Rita Paulsen alisema kwenye zawadi ya mshindi ya milioni 60, shilingi milioni 10 itatolewa kwaajili ya uongozi utakaomsimamia.

“Fainali zitafanyika Ijumaa Oktoba 9 pale King Solomon Hall karibu na ukumbi wa Nyumbani Lounge wa zamani,” alisema. “Kwenye fainali hii mshindi atapata kitita cha milioni 60 ambapo ni tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Kwa mwaka huu atapewa na mkataba wa kusimamiwa na lebo ya Tip Top Connection ambao utamwezesha kumwongoza na kuhakikisha anafanya vizuri kimuziki. Kwahiyo atatengenezewa video nzuri na kwenye audio atasaidiwa pia kuandika kama patahitajika,” aliongeza Madam Rita.

Madam Rita amesema licha ya burudani kutoka kwa washiriki hao wa BSS, kutakuwa na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Band, Navy Kenzo, Peter Msechu, Kala Jeremiah pamoja na msanii wa Nigeria anayetamba na wimbo Gallardo, Run Town.

Kiingilio kitakuwa ni elfu 25 kwa viti vya kawaida, elfu 50 viti vya VIP pamoja VVIP ambavyo vitakuwa ni laki moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents