Siasa

Rais Samia Suluhu atuma salamu za pole kifo cha Waziri wa Ulinzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesikitika na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya  aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias John Kwandikwa ambae amefariki dunia apo jana.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Rais ameandika kuwa:

“Nasikitika kuwajulisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias John Kwandikwa amefariki dunia. Nitakumbuka umahiri wake katika uongozi na uzalendo. Natoa pole kwa familia, Jeshi, Bunge na wananchi wa Jimbo la Ushetu. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents