Michezo

Rasmi: Arsene Wenger atangaza kung’atuka baada ya kuiyongoza timu hiyo kwa miaka 22 

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger sasa ametangaza rasmi kung’atuka ndani ya timu hiyo kama kocha baada ya kuiongoza kwa miaka 22.

Wenger mwenye umri wa miaka 68 amejiunga na Arsenal akitokea Nagoya Grampus Eight mwaka 1996, ameandika ujumbe wenye hisia kubwa kwa klabu na mashabiki wa timu hiyo akitangaza adhima yake ya kuondoka.

Arsenal boss Arsene Wenger announced the shock decision to step down at end of the season

Meneja huyo raia wa Ufaransa ameuwambia mtandao wa klabu hiyo kuwa baada ya kutafakari kwamakini ameamua kuachia nafasi yake ya kocha mwishoni mwa msimu huu.

Baada ya kutafakari kwa makini na mazungumzo yangu na uongozi wa klabu nadhani nimuda muafaka sasa wa mimi kujiudhuru nafasi yangu mwishoni mwa msimu.

Ninashukuru kwa kupata nafasi ya kuihudumia timu hii kwa miaka mingi, nimeiyongoza timu hii kwa moyo wangu wote.

Kwa wapenzi wote wa Arsenal kuweni makini na thamani ya timu hii. Upendo wangu na mchango wangu utakuwepo daima.

Wenger penned an emotional statement to Arsenal supporters on Friday morning

Hajawahi kutwaa taji tangu mwaka 2004 licha yakuwahi kuchukua mataji 10 muhimu na kukumbukwa kuwa meneja bora ndani ya timu hiyo.

Bilashaka wachezaji watakuwa na mshangao kwamaamuzi yaliyofikiwa na Wenger na hivyo huenda wakafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanashinda taji la Europa League kwaajili ya kumbukumbu nzuri ya kocha wao wakati wakitarajia kuwakabili Atletico Madrid mchezo wa nusu fainali Alhamisi ijayo.

Benchi la ufundi la Wenger akiwemo Gerry Peyton, Boro Primorac na Tony Colbert huwenda wakaondoka ingawa kocha msaidizi Steve Bould  huwenda akasalia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents