Afya

Rwanda yawachukulia hatua mapadri kwa kuendesha misa bila muongozo wa kuzuia corona

Mamlaka nchini Rwanda imewachukulia hatua ya kinidhamu mapadri wa Kanisa Katoliki kwa kuendesha misa bila kuzingatia muongozo wa usalama wa kuzuia maambukizo ya virusi ya corona.

Parokia ya Kanisa Katoliki la Ruhengeri kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo pia ni makazi ya mapadri hao inakabiliwa na tishio la kufungwa.

Mapadri hao, Emmanuel Ndagijimana na Felicien Nsengiyumva, wanasemekana hawakuzingatia idadi ya waumini waliotakiwa kuhudhuria misa kama iliyowekwa na serikali.

Polisi walikumbana “hali ya msongamano “katika kanisa na “kila mtu alikuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi”, kwa mujibu wa taarifa ya serikali.

“Tunawakumbusha viongozi wa kidini hasa wale waliyoruhusiwa kurejelea ibada kufuata muongozo wa usalama uliyowekwa na mamlaka husika,” taarifa hiyo ilisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents