Michezo

Serengeti Boys yaichapa Cameroon, na sasa kuelekea Gabon

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys jana (Jumapili) imefanikiwa kuichapa timu ya taifa ya vijana ya Cameroon kwa goli 1-0.

Goli hilo pekee la timu hiyo, lilifungwa katika kipindi cha kwanza na Ally Hamis Ng’anzi katika michezo uliofanyika katika uwanja wa Stade Ahmadou mjini Yaounde, Cameroon.

Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa timu hiyo ya vijana ya Tanzania, katika mechi za kimataifa za maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 yatakayoanza Mei 14 mwaka huu.

Baada ya kumaliza kambi yake nchini Cameroon Serengeti Boys itaondoka na kuelekea Gabon ambako zitafanyika fainali za michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha mataifa nane.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents