Burudani

‘Sijutii kurudi Tanzania’ – Wakazi, aeleza kwanini hakutaka kuendelea kuishi Marekani

Rapper Wakazi amesema hajutii kurudi Tanzania baada ya kukaa miaka mingi nchini Marekani alikokuwa akisoma na kufanya kazi.

10724190_1510861082495767_561653079_n

Pamoja na kukiri kuwa anakutana na vikwazo vingi katika muziki wake, Wakazi amesema uamuzi wa kurudi nyumbani ni sahihi zaidi.

“Mimi nimezaliwa na kukulia Dar es Salaam. Hivyo hapa ndio nyumbani kwetu, nje nilienda kimasomo na kutafuta maisha,” Wakazi ameiambia Bongo5. “ Siwezi kujutia kurudi nyumbani maana kwanza uzalendo wangu na uchungu wa nchi yangu usingeweza kuniruhusu kufanya hivyo. Nahitaji muziki wangu uwafikie Watanzania wote, na ni rahisi kufikia lengo hilo kama nitakuwa karibu na Watanzania hapa nyumbani badala ya kutuma nyimbo nikiwa ughaibuni.

Kuna vitu vinatokea ambavyo vinaweza kukukatisha tamaa ( setbacks & backlashes za hapa na pale) ila sio kwa kiasi cha kuhisi maamuzi yako sio sahihi, na ikumbukwe kuwa njia ya mafanikio kamwe haijanyooka,” ameongeza.

Wakazi amesisitiza kuwa maisha bora hayapatikani ughaibuni pekee. “Suala la maisha bora, halitegemei upo wapi bali jitihada binafsi za kujituma kuyapata hayo maisha bora. Speaking from experience, kuna watu Tanzania wana maisha bora zaidi ya watu wa Marekani. Hivyo hata ningelowea nchi za watu, kama nisipojituma ni kazi bure tu maana sitopata maendeleo wala mafanikio yoyote.”

Kwa upande mwingine Wakazi amezungumzia changamoto ya muziki wa Tanzania kuvuka nje ya mipaka.

“Sidhani kama kuna kasoro yoyote kwenye muziki tunaoufanya maana kiukweli muziki wa Tanzania is very diverse. Ninachoweza kusema ni tatizo kubwa la muziki kutofika au kutofanya vizuri internationally ni kwanza, jitihada za wasanii wetu ku push muziki wao bado ni ndogo sana. Pili ule muziki ambao ndio una nafasi zaidi ya kufanya vizuri haupewi kipaumbele. Pia Watanzania sio wazalendo hivyo hawawezi kutusaidia wasanii wao kufanya vizuri kwa kutupa support ya uhakika. Tayari tumeanza ku improve lakini na recognition inaongezeka, cha msingi ki kuongeza bidii na kuuboresha muziki. Nafasi bado tunayo.”

Kuhusu ujio wa studio yake, Wakazi amesema:

Studio yangu bado haijakamilika kikamilifu. Nimekuwa na majukumu mengi kidogo hivi karibuni so imekuwa ngumu kujigawa au kuweka efforts zote kwenye kitu kimoja but rather najaribu kuhakikisha projects zangu zote zina advance kwa pamoja. Sijaipa studio jina lolote kwa sasa lakini nadhani haitocheza mbali na majina ya management zangu ( workethic or cervon) Au moja ya majina yangu ya utani ila nitajitahidi jina la studio Kama ilivyo jina langu la usanii pia li represent why I stand for as an artist and as an executive. Kuhusu kusaidia wasanii wachanga, siwezi kusema kuwasaidia bali kwa wale watakaokuwa tayari kujisaidia wao wenyewe basi wanaweza kubahatika kupata mkono wa ziada kutoka kwetu. Sisi tutajali viwango na NIDHAMU ya kazi hivyo wasanii watakao onesha sifa hizo wawe wakubwa Au wachanga, studio yetu itakuwa nyumbani kwao.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents