Burudani

Sio Nedy hata mimi naweza kufanya kolabo na msanii wa WCB – Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki Ommy Dimpoz amedai licha ya yote yaliyotokea kati yake na Diamond Platnumz, lakini anaweza kuingia studio na kufanya kolabo na msanii yeyote wa WCB kama ikitokea kazi ambayo itamwitaji kufanya hivyo.

Wawili hao ambao walikuwa marafiki wa muda mrefu, waligombana na kufikia hatua ya kutupiana maneno ya kashfa kupitia mitandao ya kijamii.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Ijumaa hii, Ommy amedai kama ikitokea kazi ambayo ataona anatakiwa kufanya na msanii wa WCB basi atamtafuta kwa kuwa muziki ni biashara.

“Sio Nedy hata mimi naweza kufanya kolabo na wasanii wa WCB kwa sababu mwisho wa siku hii ni biashara, unapoona hapa anatakiwa kukaa masanii fulani unamtafuta ili kupata kitu kizuri zaidi,” alisema Ommy Dimpoz.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’ akiwa ameshirikiana na Alikiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents