Michezo

Tevez akanusha kulipwa £615,000 ‘sio vyema kuwaambia watu kuhusu kipato chako’

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Manchester city, Carlos Tevez amekanusha taarifa ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kusajiliwa kwake kwenda klabu ya Shanghai Shenhua ya China kutamfanya alipwe £615,000.

Mshahara huo ungemfanya Tevez kuwa mwanasoka anayelipwa zaidi duniani kwa sasa.

Akiongea na waandishi wa habari wiki hii kwa mara ya kwanza akiwa nchini China, Teves alisema hakuwahi kuweka wazi issue za mshahara wake.

“Baada ya mechi yangu ya mwisho nikiwa na Boca Juniours sikuwahi kuongea na vyombo vya habari kuhusu mshahara wangu” Tevez alisema.

Aliongeza, “Masuala ya mshahara ni kati yangu na mwajiri na sio na mtu mwingine, sio vyema kuwaambia watu kuhusu kipato chako,ni suala la heshima kwa wachezaji wenzangu,sina mshahara mkubwa na siwezi kusema ni kiasi gani”

Carlos Teves amehamia China rasmi,katika kuhama huko Tevez amebeba watu 19 wa familia yake na kuhamia nao nchini China.

Alisema familia yake ndio inamfanya acheze mpira vizuri na hivyo kukaa karibu na familia yake kutampa kiwango bora uwanjani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents