Burudani

The Headies: Don Jazzy na Olamide ndani ya beef kali (Video)

Don Jazzy na Olamide wametengeneza headlines kwenye tuzo za Headies 2015 nchini Nigeria.

https://www.youtube.com/watch?v=RCbYZahOsKc

Drama ilianza baada ya Reekado Banks, aliye chini ya Mavin Records ya Don Jazzy kumshinda msanii aliye lebo moja na Olamide, Lil Kesh na kushinda tuzo ya ‘The Next Rated Award.’

Alipopanda jukwaani Olamide aliamua kufunguka ya moyoni akiwa na crew nzima YBNL baada ya msanii wake Adekunle Gold kushinda tuzo ya Best Alternative.

“This award belongs to Lil Kesh. Lil Kesh is our own Next Rated artist. F**k that shit! The streets ti take over. Every f**king single was a hit back to back. From lyrically to Shoki to Efejoku. Ko ni dafun Iya anybody”, alisema Olamide, kutupa mic chini na kuondoka.

Don Jazzy aliyeshinda tuzo ya “Lifetime Achievement Award” alimjibu Olamide kwa kumuambia kama anataka gari la ushindi wa tuzo aliyoilalamika anaruhusiwa kwenda kuichukua.

“Egbon Olamide, if you want the car, come and take it,” alisema.

Kauli hiyo ilimkera Olamide aliyeamua kumporomoshea matusi Don Jazzy kwenye Twitter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents