Michezo

Timu ya watoto wa mtaani iliyoshinda kombe la dunia yatinga bungeni kupongezwa

Timu ya mpira wa miguu ya Watoto wa Mtaani ya Tanzania iliyotwaa kombe la dunia kwa watoto wa mtaani leo imetinga bungeni na kupongezwa na bunge kwa kuipa heshima Tanzania.

Tanzania-1

Akizungumza leo bungeni wakati wa matangazo, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan amesema bunge linaipongeza timu hiyo ya watoto wa mitaani kwa kuchukua ushindi huo pamoja na kuitangaza Tanzania. Pia mmoja ya wajumbe wa bunge hilo ametoa hoja kwa wabunge kuichangia timu hiyo ili kuisaidia zaidi.

Timu hiyo ilitwaa kombe la dunia kwa watoto wa mtaani baada ya kuilaza timu ya Burundi mabao 3-1 kwenye fainali iliyopigwa jijini Rio de Janeiro nchini Brazil.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents