Burudani

Video: Sebastian Mwaikambo amrithi Tandi Kathembe kwenye The Fix ya Choice FM

Aliyekuwa mtangazaji wa East Africa Radio, Sebastian Mwaikambo aka Seba the Warrior amekuwa mrithi wa Tandi Kathembe kwenye kipindi cha The Fix cha Choice FM 102.5.

“U can tell just how AWESOME #TheFIX is going to be with @SebaTheWarrior! I couldnt be more jazzed by this guy,” ametweet Tandi Jumanne hii. “It’s never easy to say goodbye but I’m so grateful for the last 5 years. All I can say is THANK YOU,” ameongeza.

bIhiTBS8
Tandi Kathembe

Seba ataanza kutangaza kipindi hicho kinachorushwa kila siku za wiki kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana, Jumatano hii

Akiongea na Bongo5 TV kuhusiana na kumrithi Tandi, Seba amesema kwa miaka mitano aliyoondesha kipindi hicho, amekifanya kuwa kipindi bora na hivyo atafanya kila jitihada kutowaangusha wasikiliza wa The Fix. “Kuingia pale sio kwamba naenda kubadilisha kila kitu bali nitaboresha yale yaliyokuwepo lakini ‘unaweka in your style’ katika nguvu yako wewe ambayo unayo. Yule ambaye alikuwepo hatoachwa na yule ambaye hakuwepo ataongezwa,” amesema.

Akiongelea kuhusu kujiunga na Choice FM, Seba amesema amekuwa akivutiwa na kituo hicho cha redio kutokana na vipindi vyake na muziki inaoucheza. “Kwanza nimefurahi, Choice FM is really a very good station. Muziki ambao wanaupiga ni wa kila aina ambao unacater kila Nyanja nikasema hapa patanifaa, lakini pia hata standard yao, maongezi yao, professionality yao mimi hapa personally nikapenda.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents